Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 29, 2024 Local time: 11:49

Nkuruma kufanyiwa mazishi rasmi miaka 50 baaya ya kifo chake


Mwanamke akipiga picha mbele ya sanamu ya aliyekuwa rais wa Ghana Kwameh Nkrumah, mjini Accra, August 7, 2019. PICHA:. REUTERS/Francis Kokoroko
Mwanamke akipiga picha mbele ya sanamu ya aliyekuwa rais wa Ghana Kwameh Nkrumah, mjini Accra, August 7, 2019. PICHA:. REUTERS/Francis Kokoroko

Chama cha upinzani nchini Ghana, cha Convention People’s Party (CPP), kimetangaza mipango ya kufanya upya mazishi ya kiongozi mwanzilishi wa taifa hilo Kwame Nkrumah, yatakayofanyika mwezi November.

Chama hicho kilichoongoza Ghana baada ya uhuru, kimesema kwamba Nkrumah hakupewa mazishi ya heshima yanayostahili kupewa kiongozi wa taifa.

Nkuruma alifariki April mwaka 1972, miaka 50 iliyopita, alipokuwa anatibiwa nchini Romania, na chama chake kinasema kwamba roho yake haijapumzika kwa amani.

Alizikwa katika kijiji cha Nkroful kusini mwa Ghana.

Mabaki yake yalisafirishwa baadaye na kuzikwa katika jengo la makumbusho katika mji mkuu wa Accra.

Bila ya kutoa maelezo zaidi iwapo mabaki ya Nkuruma yatafukuliwa tena, Chama cha CPP kimesema kwamba kitazindua ratiba hivi punde ya kufanyika rasmi mazishi yake.

XS
SM
MD
LG