Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 12:22

Njia ya wahamiaji kuendelea kufungwa Austria


Kijana akishiriki katika mgomo uliofanywa na wakimbizi na wahamiaji mbele ya uzio wa waya unaotenganisha Ugiriki na Macedonia.
Kijana akishiriki katika mgomo uliofanywa na wakimbizi na wahamiaji mbele ya uzio wa waya unaotenganisha Ugiriki na Macedonia.

Njia ya wahamiaji ya Balkan itaendelea kufungwa baada ya Slovania, Macedonia, Serbia na Croatia kufunga mipaka wiki hii kwa wahamiaji wote.

Waziri wa mambo ya ndani wa Austria, Johanna Mikl-Leitner anasema njia ya wahamiaji ya Balkan itaendelea kufungwa baada ya Slovania, Macedonia, Serbia na Croatia kufunga mipaka wiki hii kwa wahamiaji wote wanaopanga kutafuta hifadhi ndani ya mipaka yao.

Mikl-Leitner ameliambia na gazeti la kila siku la Ujerumani la Die Welt leo kwamba njia ya Balkan kupitia nchi zote itaendelea kufungwa na kusema hawatarudi nyuma kwa uamuzi huo.

Wakati huohuo shirika la habari la Uturuki linasema wahamiaji watano, ikijumuisha mtoto mchanga wa miezi mitatu, wamezama katika ufukwe wa magharibi wa Uturuki baada ya boti iliyokuwa imewabeba kuelekea Uguriki kuzama ikiwa njiani kuelekea kisiwa cha Lesbos.

XS
SM
MD
LG