Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 17, 2024 Local time: 16:01

Mzozo wa ukosefu wa chakula waongezeka Nigeria


Mtoto katika kambi ya walopoteza makazi yao ya Yola, jimbo la Adamawa.
Mtoto katika kambi ya walopoteza makazi yao ya Yola, jimbo la Adamawa.

Umoja wa mataifa unaeleza kuwa maelfu ya watoto wako kupoteza maisha kwa ajili ya mzozo wa chakula uanongezeka katika eneo lilokumbwa na vita la kaskazini mashariki mwa Nigeria. Dharura hiyo inatokea wakati mbaya kwa Nigeria ambayo uchumi wake umeathirika kutokana na bei ndogo ya mafuta na kupungua kwa uzalishaji wa mafuta.

Miaka mingi ya mapigano baina ya vikosi vya usalama na wanamgambo wa Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria, kumevuruga mavuno na kuharibu masoko na kuacha baadhi ya sehemu kuwa hazipitiki kuwezesha kufikishwa kwa misaada ya kibinadam.

Matatizo yameongezeka na kuwa mzozo wa chakula ambao unawaacha watoto katika kanda hiyo kuwa hatarini Zaidi, kwa mujib wa mratibu wa kikanda wa misaada ya umoja mataifa bw Toby Lanzer.

Bw. Lanzer anasema, tuna watoto takriban elfu 250 katika eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria ambao wanautapia mlo mbaya na tunaweza kupoteza hadi watoto elfu 50 kabla ya mwisho wa mwaka iwapo hatutaongeza msaada sasa hivi.

Lanzer anasema Nigeria inahitaji dola millioni 164 katika miezi 3 ijayo kusaidia watoto na zaidi ya millioni 4 nyengine katika nchi ambayo inakabiliwa na ukosefu mbaya wa usalama wa chakula.

Wiki ilopita, mtandao wa kutoa onyo kwa ajili ya njaa ulieleza kuwa maeneo ya kaskazini mashariki huwenda tayari yanakabiliwa na njaa.

Nigeria imekuwa ikikabiliana na harakati za waasi wa Boko Haram kwa miaka 7 sasa.

Bw Lanzer anasema, hali ya kifedha ya Nigeria ni tete. Na kutarajia Nigeria kusaidia katika kiwango kinachohitajika itakuwa ni ombi kubwa sana kutoka jumuiya ya kimataifa.

Uchumi wa Nigeria unategemea mauzo ya nje ya mafuta na kushuka kwa bei za mafuta duniani pamoja na mashambulizi ya wanamgambo kwenye mabomba ya mafuta katika eneo la kuzalisha mafuta la Niger Delta, kumepunguza mapato yanayoingia kwenye hazina za Nigeria.

Uchumi ulishuka katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka, na mwakilishi wa taifa hilo kwenye shirika la fedha duniani IMF, aliiambia mtandao wa habari wa Bloomberg News kuwa uchumi huwenda ukapungua mwaka huu mzima.

Kuchangia matatizo hayo, ni watu waliopoteza makazi wanaoishi kwenye kambi inaendelea kuongezeka kwa sababu jeshi limekombowa jamii ambazo zilikuwa chini ya udhibiti wa Boko Haram.

Mratibu wa idara ya kitaifa ya dharura huko kaskazini mashariki, Muhammed Kanar anasema wengi wa walowasili wanakuja kutoka maeneo yasio na chakula au matibabu, na wananjaa pale wanapowasili.

Kanar alitowa mfano wa kambi ya watu walopoteza makazi katika mji wa Monguno. Kambi hivi karibuni ilikuwa kutoka watu elfu 4 hadi elfu 30. Anatarajia idadi hiyo kuongezeka.

XS
SM
MD
LG