Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 01:04

Uchumi wa Nigeria wadorora


sarafu ya Nigeria
sarafu ya Nigeria

Nigeria inaelekea katika hali ya kudorora kwa uchumi.

Magavana wa benki kuu ya Nigeria wanakutana licha kuwa mtazamo wa kifedha wa uchumi mkubwa barani Afrika unaonekana kudumaa. Takwimu zilotolewa wiki iliyopita zinaonyesha uchumi wa taifa hilo ukishuka. Wachumi wanalaumu uhaba wa mafuta, kukatika mara kwa mara kwa umeme, na kushuka kwa uzalishaji mafuta ambao ni pato kuu la Nigeria.

Nigeria inaelekea katika hali ya kudorora kwa uchumi.

Hio ndio sababu wachambuzi , baada ya idara ya taifa ya takwimu ilipotangaza kuwa uchumi umepunguwa kwa nne ya kumi ya asilimia katika robo ya kwanza ya mwaka huu .

John Ashbourne mchumi wa Afrika katika shirika la Capital Economics lenye mako yake mjini London, anasema uhaba wa mafuta na fedha za kulipia bidhaa zinazoagizwa kutoka nje, kumedumaza ukuwaji wa uchumi. Anasema hadhani kuwa kipindi cha robo ya pili kitakuwa na ahuweni.

Bw Ashborne anasema, kuna uwezekano mkubwa kuwa uchumi utasinyaa tena katika kipindi cha robo hii, na baada ya hapo tutakuwa katika hali ya kudorora kwa uchumi.

Mafuta ndio bidhaa kuu ya Nigeria wanayouza nje ni mfadhili mkuu wa bajeti ya serikali. Kushuka kwa bei za mafuta ghafi duniani kumepunguza mapato na kuumizauchumi.

Vilevile uzalishaji wa mafuta umeshuka kwa takriban mapipa nusu millioni kwa siku kwa sababu wanamgambo walilipua mabomba kadhaa ya mafuta katika eneo linalozalisha mafuta la Niger Delta.

Ashborne anasema serikali haijasaidia hali kwa kuweka udhibiti kwa ubadilishaji wa fedha za kigeni na hivyo kupelekea uhaba wa dola nchini.

Upungufu huo wa dola unaathari kadhaa ikiwa ni pamoja na upungufu wa petroli, kwa sababu Nigeria inauza nje mafuta yake mengi.

Ukuwaji pia katika uzalishaji viwandani pia umepungua katika kipindi cha robo ya kwanza. Ashborne anasema wazaishaji ambao wanategemea vifaa kutoka nje hawawezi kuvipata.

Wengi wameiomba benki kuu kushusha thamani ya sarafu ili kuchochoea ukuwaji na kumaliza uhaba wa dola. Rais Muhammadu Buhari anasema yeye hapendelei hilo.

Hata hivyo bado wanasubiri kuona iwapo maafisa wa benki kuu watachukuwa hatua yeyote baada ya kumaliza mkutano wao huko Abuja hivi leo.

XS
SM
MD
LG