Nigeria tayari imehaspokea dozi milioni 2 za chanjo ya Johnson & Johnson kutoka Finland, Ugiriki na Slovenia huku zaidi ikitarajiwa kutoka nchi za Umoja wa Ulaya.Faisal Shuaib, mkuu wa Wakala wa Kitaifa wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (NPHCDA), amesema kwamba lengo la Nigeria ka kuchanja asilimia 70 ya watu wake na kwamba sasa hilo litawezekana kutokana na mchango wa Uhispania.
Shuaib alisema 23.4 ya watu wanaostahili wamepata dozi ya kwanza ya chanjo, wakati asilimia 15.8 wakiwa wamechanjwa kikamilifu dhidi ya virusi vya corona. Nigeria imerekodi kesi 255,937 zilizothibitishwa kufikia Jumanne na vifo 3,143 tangu janga hilo kuzuka miaka miwili iliyopita.