Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 28, 2023 Local time: 23:36

Nigeria yaanza mipango ya kuwaondoa raia wake waliokwama katika nchi jirani za Ukraine


Wakimbizi kutoka Ukraine wakipiga foleni kusubiri kuingia Poland. Picha ya AFP, Februari 28, 2022
Wakimbizi kutoka Ukraine wakipiga foleni kusubiri kuingia Poland. Picha ya AFP, Februari 28, 2022

Serikali ya Nigeria imeanzisha leo Jumatano mpango wa kuwaondoa raia wake waliokwama katika nchi jirani za Ukraine, baada ya raia hao kukimbia uvamizi wa Rashia.

Nchi za Kiafrika zimekabiliwa na changamoto ya kusaidia raia wake waishio Ukraine ambao walivuka mpaka kuelekea Poland, Roumania, na Hungary, haswa baada ya taarifa kwamba baadhi yao walidhulumiwa na kuzuiliwa mpakani.

Ndege za kusafirisha raia hao wa Nigeria zilikuwa zinatarajiwa kuondoka leo, zikiwa na uwezo wa kurejesha nyumbani watu 1,300 kutoka Poland, Roumania na Hungary, wizara ya mambo ya nje ya Nigeria imesema katika taarifa.

Katibu mkuu kwenye wizara ya mambo ya nje ya Nigeria Gabriel Adula amesema “ Kundi la kwanza la walioondolewa kutoka nchi hizo jirani za Ukraine linatarajiwa kuwasili Nigeria Alhamisi”.

Balozi wa Ukraine nchini Afrika Kusini alisema wiki hii kwamba kuna wanafunzi 16, 000 kutoka Afrika nchini mwake, lakini wengi ni kutoka nchi ambazo hazina ubalozi nchini Ukraine, na hivo kufanya hali kuwa ngumu.

Wizara ya mambo ya nje ya Nigeria inasema kuna wanafunzi 5,600 wa Nigeria huko Ukraine.

XS
SM
MD
LG