Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 14:44

Nigeria: Waumini 25 wa kanisa la Kibatista watekwa nyara na watu wenye silaha


Wanaume watatu, waliotambulishwa kama watekaji nyara wa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Bethel Baptist nchini Nigeria, Septemba 23, 2021.
Wanaume watatu, waliotambulishwa kama watekaji nyara wa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Bethel Baptist nchini Nigeria, Septemba 23, 2021.

Watu wenye silaha walishambulia kanisa la Kibatista kaskazini magharibi mwa Nigeria na kuwateka nyara waumini 25 waliokuwa katika ibada ya Jumapili, kiongozi mkuu wa kanisa hilo alisema Jumatatu.

Shambulio hilo ni utekaji wa hivi karibuni wa watu wengi nchini Nigeria, ambako ukosefu wa usalama ni moja ya changamoto kubwa zinazomkabili rais mpya Bola Tinubu, ambaye atachukua hatamu za uongozi mwishoni mwa mwezi huu.

Washambuliaji Jumapili walivamia kanisa la Kibatista la Bege katika eneo la Chikun katika jimbo la Kaduna, awali wakiwateka nyara watu 40, ingawa 15 walifanikiwa kutoroka baadaye, mchungaji Joseph Hayab, mkuu wa chama cha Wakristo wa Nigeria katika jimbo la Kaduna, ameiambia AFP.

Msemaji wa polisi wa Kaduna amethibitisha shambulio la Jumapili lakini hakuweza kutoa maelezo zaidi.

Magenge ya wahalifu wenye silaha nzito wanaojulikana kama majambazi mara kwa mara huwateka nyara watu wengi kaskazini magharibi na katikati mwa Nigeria ili kulipwa fidia, na kuwashikilia mateka wao katika kambi ambazo ziko mafichoni ndani ya misitu mikubwa inayopatikana katika eneo lote hilo.

XS
SM
MD
LG