Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 01:37

Nigeria: watu 50 wauawa katika shambulio kwenye kanisa la kikatoliki


Wabunge wanasema zaidi ya watu 50 wanahofiwa kuuawa katika shambulio kwenye kanisa la mtakatifu Francis katika mji wa Owo, June 5, 2022. Picha ya AP
Wabunge wanasema zaidi ya watu 50 wanahofiwa kuuawa katika shambulio kwenye kanisa la mtakatifu Francis katika mji wa Owo, June 5, 2022. Picha ya AP

Watu wenye silaha walishambulia kanisa moja ya kikatoliki kaskazini magharibi mwa Nigeria wakati wa ibada ya Jumapili, na kuua takriban watu 50 wakiwemo wanawake na watoto, kwa mujibu wa daktari wa hospitali na ripoti za vyombo vya habari.

Vyombo kadhaa vya habari vya Nigeria vimesema watu hao wenye silaha walifyatulia risasi waumini na kulipua mabomu kwenye kanisa la mtakatifu Francis katika mji wa Owo. Washambuliaji hawakutambulika na nia yao haikufahamika mara moja.

“Inasikitisha sana kwamba wakati misa takatifu ikiendelea, watu wenye silaha wasiojulikana walishambulia kanisa la mtakatifu Francis, watu wengi wanaohofiwa kuuawa na wengine kujeruhiwa na kanisa kuvamiwa,” alisema msemaji wa kanisa katoliki nchini Nigeria, mchungaji Augustine Ikwu.

XS
SM
MD
LG