Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 07, 2023 Local time: 01:28

Upigaji kura wamalizika Nigeria, Hesabu zaanza


Afisa wa tume ya uchaguzi Nigeria akigagua masanduku ya kura, March 29, 2015.

Upigaji kura ulimalizika Nigeria Jumapili na maafisa wameanza kazi kubwa ya kuhesabu kura, siku moja baada ya matatizo ya kiufundi katika mfumo mpya kusababisha kuongezwa kwa siku moja katika upigaji kura.

Attahiru Jega, mkuu wa tume ya uchaguzi, aliwaambia waandishi wa habari kuwa hesabu ya kura kutoka katika majimbo yalitazamiwa kuwasili Abuja baadaye Jumapili.

Akiwa anatafuta awamu mpya ya uongozi Rais Goodluck Jonathan anapambana vikali na kiongozi wa zamani wa kijeshi Muhammadu Buhari.

Maafisa uchaguzi walisifu mfumo mpya wa BVR kuwa utazuia kabisa wizi wa kura ambao umekumba chaguzi zilizopita. Hata hivyo mfumo huo ulionyesha hitilafu kadha zilizosababisha upigaji kura kuongezwa kwa siku moja zaidi.

Wafuatiliaji uchaguzi kutoka Umoja wa Afrika na Jumuiya ya ECOWAS walisema Jumapili kuwa licha ya ucheleweshaji na matatizo ya kiufundi na ghasia za hapa na pale, uuandaaji wa uchaguzi "unakubalika."

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon pia aliipongeza Nigeria kwa uchaguzi huo akisema amevutiwa na "nia na uvumilivu" wa Wanigeria katika kutaka kushiriki katika uchaguzi huo.

XS
SM
MD
LG