Washukiwa wa kundi la kigaidi la Boko Haram wameshambulia miji miwili ya kaskazini mwa Nigeria, jana Jumatano kwa mabomu kadhaa ya kujitoa muhanga, maguruneti na ufyatuaji risasi na kuua watu 50. Mlipuko wa kwanza wa Jumatatu ulitokea katika msikiti wa kitongoji cha mji wa Maiduguri.