Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 22, 2024 Local time: 13:26

Nigeria: Polisi wanawatafuta watekaji nyara


Waandamanaji wakilalamikia utekaji nyara wa makundi ya waoiganaji nchini Nigeria
Waandamanaji wakilalamikia utekaji nyara wa makundi ya waoiganaji nchini Nigeria

Polisi nchini Nigeria wanawatafuta washukiwa katika tukio la kumteka nyara kiongozi wa kanisa la Methodist nchini humo, aliyeachiliwa baada ya kulipa dola 240,600.

Samuel Kanu Uche, aliachiliwa huru jumatatu, siku moja baada ya kutekwa nyara mjini Abia, kusini mashariki mwa Nigeria.

Msemaji wa polisi Geoffrey Ogbonna, amesema kwamba maafisa wa usalama wanawatafuta washukiwa waliomteka nyara Uche.

Kulingana na shirika la ujasusi la mjini Lagos, SBM, Matukio ya utekaji nyara yameongezeka nchini Nigeria, na kiasi cha dola milioni 18 zimelipwa kati yam waka 2011 na 2020 ili kuhakikisha kwamba waliotekwa nyara wanaachiliwa huru.

Serikali ya Nigeria imekuwa ikitunga sheria kali dhidi ya utekaji nyara, ikiwemo kupiga marufu malipo kwa watekaji nyara, kama mbinu ya kukabiliana na matukio hayo.

XS
SM
MD
LG