Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 00:05

Kushuka kwa bei za mafuta zaathiri uchumi kwa wazalishaji


visima vya mafuta

Rais Muhammadu Buhari alishinda uchaguzi mwaka jana akiahidi kubadilisha utajiri wa Nigeria.

Kuporomoka kwa bei za mafuta kumeteremsha uchumi wa nchi nyingi zinazosafirisha mafuta, na mzalishaji mkubwa wa mafuta barani Afrika, Nigeria nayo pia imekumbwa na hali hio.

Mafuta yanachangia takriban asilimia 70 ya pato la serikali ya Nigeria, na inachangia takriban asli mia 69 ya pato lake la usafirishaji nje. Lakini sio kama ilivyokuwa. Katika miaka ilopita, mafuta ilikuwa yakiuzwa dola mia kwa pipa, lakini bei sasa imeanguka na kufikia dola 35 kwa pipa. Kushuka kwa bei kumewatia wasiwasi wachambuzi.

Bismarck Riwane ni mchambuzi wa masuala ya fedha anasema hatari ya kuporomoka kwa bei ya mafuta ni janga kubwa ikiangaliwa katika mtazamo wa kujiandaa na janga hilo.

Rais Muhammadu Buhari alishinda uchaguzi mwaka jana akiahidi kubadilisha utajiri wa Nigeria. Alipendekeza bajeti inayozidisha matumizi kwa takriban robo na kuwekeza katika miundo mbinu.

Uwekezaji huo unahitajika kote nchini Nigeria, hususan kaskazini mashariki ambako wanamgambo wa Boko Haram wamechoma moto miji na kuharibu vijiji.

XS
SM
MD
LG