Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 15:40

Rais wa Nigeria kuzuru Marekani


Rais wa Nigeria Nuhammadu Buhari
Rais wa Nigeria Nuhammadu Buhari

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameanza ziara yake ya siku nne mjini Washington Jumapili, ambako anatarajiwa kufanya mazungumzo na rais wa Marekani Barack Obama.

Tishio lililoletwa na kundi la wanamgambo la Boko Haram, linatarajiwa kuwa juu kwenye ajenda ya mazungumzo, pale rais Obama anapomkaribisha kiongozi wa Nigeria kwenye ikulu ya White House kwa mara ya kwanza Jumatatu.

Marekani inataka kupanua msaada wake kwa Nigeria katika kupambana na wanamgambo hao wa Boko Haram, ambao wameongeza mashambulizi yao tangu Rais Buhari alipoingia madarakani mwezi Mei.

XS
SM
MD
LG