Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 04, 2023 Local time: 15:50

Nigeria imefunga mpaka wake na Benin kuzuia usafirishaji magendo wa mchele


Usafirishaji magendo wa mchele umepelekea Nigeria kufunga mpaka wake na Benin

Rais Buhari wa Nigeria alisema kutakuwa na mkutano wa pamoja na majirani zake wa eneo la kaskazini Benin na Niger ili kuzungumzia hatua za kuchukuliwa kudhibiti biashara ya magendo kuvuka mipaka yao

Serikali ya Nigeria ilieleza Jumatano inafunga sehemu ya magharibi ya mpaka wake na Benin ili kuzuia usafirishaji magendo wa mpunga ambao unatishia juhudi za nchi hiyo kuimarisha uzalishaji wa ndani.

Nchi hiyo inataka kuwa inajitegemea yenyewe katika uzalishaji mpunga na imeweka masharti ya uingizaji mchele lakini jambo hilo limesababisha bei kupanda na kupelekea usafirishaji kwa njia ya magendo kutoka Benin kuingia Nigeria.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari alianzisha sera tangu alipoingia madarakani mwaka 2015 ambazo zina lenga kusitisha uingizaji mchele nchini humo ili kuimarisha uzalishaji wa ndani na kulinda akiba ya fedha za kigeni.

Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari
Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari

Alisema usafirishaji mchele kwa njia ya magendo kupitia mpaka wa magharibi umetishia sera yake ya nchi kujitegemea yenyewe bila msaada wa nje. Rais Buhari alikaririwa akisema katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake kwamba nchi imeweka akiba kubwa ya fedha za kigeni kutokana na sera yake badala ya kuzitumia fedha chache za kigeni kuagizia mchele kutoka nje. Alisema hawawezi kuruhusu usafirishaji haramu wa bidhaa katika kiwango hicho kuendelea. Taarifa hiyo haikusema ni lini sehemu ya mpaka huo ulifungwa.

Serikali inasema uingizaji mpunga na ngano nchini Nigeria kwa pamoja unagharimu takribani dola bilioni nne kwa mwaka lakini watu wake milioni 190 wanategemea bidhaa zinazoagizwa kutoka nje kwa sehemu kubwa ya mahitaji yao kutokana na upungufu wa uwezo wa uzalishaji nchini humo kutokana na kidhibiti cha uwezo wa uzalishaji.

Nigeria inafikiria kukuza kilimo kwa ajili ya kupeleka bidhaa nje ya nchi ili kupata fedha zaidi na kuongeza mapato kutoka nje ya eneo lake lenye utajiri wa mafuta.

XS
SM
MD
LG