Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 23, 2024 Local time: 07:56

Nigeria yamshitaki Dick Cheney


Dick Cheney, makamu rais wa zamani wa Marekani
Dick Cheney, makamu rais wa zamani wa Marekani

Idara ya kupambana na rushwa nchini Nigeria imefungua mashtaka dhidi ya makamu wa zamani wa rais wa Marekani Dick Cheney, kuhusiana na kadhia za hongo zinazoihusisha kampuni ya nishati ya Halliburton.

Waendesha mashtaka walifungua mashtaka 16 dhidi ya Cheney, ambaye alikuwa mkuu wa Halliburton, kabla hajawa makamu rais, na maafisa wengine kadhaa wa zamani na wa sasa wa kampuni hiyo, siku ya Jumanne kwenye mahakama kuu mjini Abuja. Maafisa wanasema watendaji hao wanashtakiwa kwa kupanga na kwa mujibu wa nyaraka za mahakama, kutoa hongo kwa maafisa wa serikali.

Madai yanatokana na shutuma ambapo kampuni ya mafuta ya Halliburton na matawi yake, KBR walitoa hongo ya zaidi ya dola milioni 180 kati ya mwaka 1995 na 2005 kushinda ukandarasi wa kujenga viwanda vya gesi ya asili nchini Nigeria. Halliburton inakanusha kuhusika na mwanasheria wa Cheney anasema shutuma hizo hazina msingi.

Cheney alikuwa mkurugenzi mkuu wa Halliburton kutoka mwaka 1995 hadi mwaka 200 kabla hajachaguliwa kuwa makamu rais katika utawala wa zamani wa Rais wa Marekani George W.Bush. Mwaka jana KBR ililipa fidia ya dola milioni 577 kwa idara ya sheria ya Marekani na idara ya usalama ya Marekani kwa madai tofauti yaliyohusiana na kadhia hizo.


XS
SM
MD
LG