Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 19:18

Niger yaanza kuhesabu kura


Rais wa Niger Mahamadou Issoufou akijiandaa kupiga kura yake.
Rais wa Niger Mahamadou Issoufou akijiandaa kupiga kura yake.

Takriban wagombea wengine 14 walikuwa wakishindana kupata urais na Issoufou akiwemo Seyni Oumarou ambae ni kiongozi wa upinzani.

Zoezi la kuhesabu kura limeanza Niger baada ya uchaguzi wa rais na bunge kukamilika Jumapili.

Matokeao yanatarajiwa kutolewa baadaye wiki hii. Mahamadou Issoufou anawania muhula wa pili wa kipindi cha miaka 5 akitoa ahadi ya kuangamiza wanamgambo wa kiislamu na pia kuimarisha moja ya mataifa masikini kabisa duniani.

Takriban wagombea wengine 14 walikuwa wakishindana kupata urais na Issoufou akiwemo Seyni Oumarou ambae ni kiongozi wa upinzani.

Wengine kutoka vyama ya upinzani ni pamoja na Hama Amadou ambae wakati mmoja aliwahi kukamatwa kwa tuhuma za kufanya biashara ya usafirisgaji haramu wa watoto.

Wakosoaji wa Issoufou wanasema kuwa alitumia ukandamizaji kabla ya upigaji kura kwa kuwakamata wafuasi wa vyama vya upinzani, wanasiasa, waandishi wa habari na hata mwana mziki alietoa wimbo wa kumkosoa.

Rais Issoufou ameliambia shirika la habari la FP kuwa ana uhakika wa kushinda kwenye uchaguzi huo akiongeza kuwa haoni uwezekano wa kufanyika kwa uchaguzi wa marudio.

XS
SM
MD
LG