Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 07:08

Polisi 3 wauwawa Niger katika shambulizi la mpakani


Amadou Djibo Ali, kiongozi wa upinzania nchini Niger.
Amadou Djibo Ali, kiongozi wa upinzania nchini Niger.

Polisi watatu wameuwawa katika shambulizi dhidi ya wanajeshi wa usalama wa Niger karibu na mpaka na Nigeria, Burkina faso na mali. Wizara ya ulinzi ya Niger imetoa taarifa kwenye televisheni ya umma hapo alhamisi.

Kanali Ledru Moustapha amesema katika taarifa kwamba shambulizi lilifanywa na washambuliaji ambao waliwasili kwenye pikipiki nne na gari moja aina ya Toyota.

Katika shambulizi la awali, wanajeshi watatu jeshi la Niger walijeruhiwa na wajitoa mhanga watano waliuwawa jumatano katika shambulizi la kushtukiza katika wilaya ya Diffa, ambapo maafisa wanalilaumu kundi la Boko haram. Mashambulizi yametokea ikiwa ni siku chache kabla ya wapiga kura wa Niger kwenda kupigia kura siku ya jumapili kwa ajili ya duru ya pili ya uchaguzi wa rais .

Msemaji wa muungano wa upinzani Amadou Bjibo anawaomba wafuasi wake wagomee kupiga kura.Upinzani inasema upigaji kura wa Februari 21 uligubikwa na wizi wa kura.

XS
SM
MD
LG