Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 03:19

Niger kumpa hifadhi mtoto wa Gadhafi


Saadi Gaddafi, mtoto wa kiume wa kiongozi wa zamani wa Libya Muammar Gaddafi, akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Tripoli, January 31, 2010.

Saadi Gadhafi kupewa hifadhi kwasababu za kibinadamu

Niger imetangaza kwamba itampatia hifadhi mtoto wa kiume wa kiongozi wa zamani wa Libya Moammar Gadhafi.

Rais wa Niger, mahamadou Issoufou amesema kuwa Saadi Gadhafi ambaye alikimbia Libya mwezi August, atapewa hifadhi kwa sababu za kibinadamu.

Baraza la taifa la mpito la Libya linataka Saadi Gadhafi ashtakiwe kwa uhalifu anaotuhumiwa ameutenda wakati alipokuwa akiongoza shirikisho la mpira wa miguu nchini humo.

Kaka yake Saadi, Seif al-Islam anatakiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa upinzani dhidi ya utawala wa baba yake.

Rais Issoufou anasema Seif hayuko nchini Niger na hakuna maamuzi yaliyofanywa kuhusu jinsi watakavyolishughulikia suala lake pindi atapowasili nchini humo.

XS
SM
MD
LG