Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 16:15

Serikali ya kijeshi ya Niger yatoa tahmini ya mapambano na rushwa.


Wanajeshi wa Niger.
Wanajeshi wa Niger.

Serikali ya kijeshi ya Niger imesema juhudi za kupambana na ulaji rushwa zinaongozwa na tume yenye wajumbe 40 ikiwa ni ya kijeshi , wataalamu wa kodi na wahasibu ambao wanajaribu kurejesha fedha ambazo zinaweza kuwa zimeibiwa wakati wa utawala wa rais Tandja.

Serikali ya kijeshi ya Niger imesema juhudi za kupambana na ulaji rushwa zinaongozwa na tume yenye wajumbe 40 ikiwa ni kijeshi , wataalamu wa kodi na wahasibu ambao wanajaribu kurejesha fedha ambazo zinaweza kuwa zimeibiwa wakati wa utawala wa rais Tandja.

Msemaji wa serikali mahaman laouali dandah amesema kuna ushahidi wa kutosha kwamba rushwa ni sehemu muhimu ya kufanya biashara huko Niger.

Dandah amesema kuna hali jumla ya ulaji rushwa nchini humo . hata Mradi wa changamoto ya millennium wa marekani MCA ulifanya utafiti katika sehemu ya vita dhidi ya rushwa huko niger na ilisema kuwa kuna baadhi ya udhaifu katika juhudi hizo. Dandah amesema udhaifu huo uliizuiya Niger kuwa na sifa za kuingia katika mradi wa MCA wakati wa utawala wa tandja.

Bagna Aissata Fall ni mjumbe wa baraza la mpito la mashauriano la Niger na aliongoza tawi la kundi la kimataifa la kupambana na rushwa Transparency International. Amesema ni mapema sana kusema kama kumekua na mabadiliko muhimu katika kupambana na rushwa lakini anaamini kwamba hatua za jeshi mpaka sasa zina tia moyo.

Fall amesema tume mpya ni njia moja ya jumuiya ya kiraia kupima dhamira halisi ya jeshi kupambana na rushwa. Lakini amesema hawawezi kupata sifa za bure. Anataka kuona hatua zinachukuliwa kupinga rushwa na akasema kwamba hatua hiyo ni lazima iwe ya kweli na siyo hotuba za kisiasa.

Fall amesema ana matumiani na tume hiyo lakini anasubiri kuona itakavyofanya kazi. Tume zilizopita zilizuiliwa kwa kuingiliwa kisiasa kwa hiyo anatarajia kwamba jeshi halitaingilia kati kazi yake.

Ikiwa imebakia chini ya mwaka mmoja kufanyike uchaguzi mpya katika moja kati ya nchi masikini duniani msemaji wa serikali dandah amesema jeshi linatarajia kuandaa serikali mpya ya kiraia itakayofuata njia bora zaidi.

Dandah amesema kipindi hichi cha mpito ni nafasi ya kutuma ujumbe mkali wa kuanza mageuzi muhimu. Mara kazi hiyo itakapoanza amesema itakuwa na uungwaji mkono wa wananchi kwa sababu vita dhidi ya rushwa ni suala muhimu kwa watu wa Niger. Na mara watu watakapomiliki mpango huu hawataruhusu serikali ya baadae kurejesha rushwa.

Chama kikubwa cha upinzani cha Niger kinaeelezea hofu juu ya tume mpya kikisema kuwa juhudi zilizopita za kutokomeza rushwa zilikuwa porojo tu kuliko utekelezaji thabiti wa sheria.

XS
SM
MD
LG