Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 10:21

Ni asilimia mbili pekee ya watu Africa waliopata chanjo za Covid


Watu wakitembea kwenye barabara za Lagos, Nigeria
Watu wakitembea kwenye barabara za Lagos, Nigeria

Shirika la afya duniani limesema Alhamisi kwamba ni takriban asilimia mbili pekee ya watu barani Afrika ambao wamepokea chanjo za covid.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, mataifa 15 kati ya jumla ya mataifa 54barani yamechanja takriban asilimia 10 ya watu wake na kwa hivyo kufikia vingango vilivyo kusudiwa kufikia mwisho wa Septemba.

Mratibu wa chanjo barani Afrika kutoka shirika la afya dunia Richard Mihingo amesema kwamba kuna hatua zilizopigwa ingawa kuna safari ndefu kuelekea kuchanja asilimia 40 ya watu wake kufikia mwishoni mwa mwaka huu. Muhingo ameongeza kusema kwamba upelekaji wa chanjo barani humo umeongezeka lakini mifumo hafifu ya usambazaji ni changamoto kubwa.

Jumla ya chanjo milioni 23 zimewasili Afrika Septemba, ikiwa ni ongezeko mara 10 kulinganishwa na mwezi Juni. Nusu ya mataifa 52 ya kiafrika yaliopokea chanjo hizo ndiyo pekee yaliotoa chanjo kamili kwa asilimia 2 ya watu wake. Hata hivyo visiwa vya Mauritius na Seychelles vimefaulu kuchanja asilimia 60 ya watu wake kulingana na data za WHO.

Morocco imetoa chanjo kamili kwa asilimia 48 ya watu wake. Mataifa mengine ambayo yamepita asilimia 20 ni Tunisia, Comoros na Cape Verde.

XS
SM
MD
LG