Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 16:07

New York Times yachapisha nakala ya ulipaji kodi ya 1995 ya Trump


Mgombea urais wa Republican, Donald Trump
Mgombea urais wa Republican, Donald Trump

Maafisa wa kampeni za wagombea urais Marekani, Hillary Clinton na Donald Trump, walishutumiana kila mmoja baada ya gazeti la New York Times kuandika kile kinachoonekana kuwa fomu ya malipo ya kodi ya serikali kuu ya mwaka 1995 ya mgombea wa Republican, Donald Trump.

Hati hizo zilizotumwa kwa gazeti la New York Times zinaonesha Trump alieleza kupata hasara ya dola milioni 916 katika biashara zake mwaka 1995 jambo ambalo lilimwezesha bilionea huyo kutolipa kodi ya mapato kwa miaka kadhaa.

Kutolewa hadharani kwa hati hizo inafuatia siku kadhaa baada ya mgombea wa Democratic, Hillary Clinton, kumkosoa Trump juu ya kutotangaza hati za ulipaji kodi wake kutiokana na mapato yake ya mwaka, wakati wa mdahalo wao wa kwanza wa kampeni za kugombania kiti cha rais uliofanyika mwishoni mwa mwezi uliopita.

Hata hivyo wasaidizi wa Trump siku ya Jumapili walimtetea mgombea wa Republican juu ya shutuma hizo za ulipaji kodi kupitia kwenye vyombo kadhaa vya habari.

XS
SM
MD
LG