Upatikanaji viungo

Netanyahu kuanza ziara katika nchi nne za Afrika


Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anatazamiwa kuanza ziara yake katika nch i nne za bara la Afrika Jumatatu, akiwa anatafuta washirika wapya wa kibiashara barani Afrika.

Ingawa ratiba maalum haijatolewa Netanyahu anatazamiwa kuanza ziara yake nchini Kenya Jumatatu na baadaye kutembelea Uganda, Kenya, Ethiopia na Rwanda.

Ziara hiyo pia inaambatana na siku ya kuadhimisha miaka 40 tangu tukio la kuokolewa mateka wa kiyahudi katika uwanja wa ndege wa Entebbe, Uganda ambapo kaka yake Netanyahu aliuawa,Julai 4, 1976.

Mchambuzi wa Masuala ya siasa kutoka jimbo la South Carolina , Marekani anaeleza juu ya umuhimu wa ziara hiyo.

Ziara hiyo inakuja huku Israel ikiwa inazindua mpango wa msaada wa mamillioni ya dolla kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na nchi za afrika.

XS
SM
MD
LG