Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 20, 2025 Local time: 22:02

Netanyahu ayaponda mashauriano ya Marekani na Iran


Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu akizungumza mbele ya bunge la Marekani mjini Washington, Machi 3, 2015.
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu akizungumza mbele ya bunge la Marekani mjini Washington, Machi 3, 2015.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema mashauriano yanayoendelea kati ya Marekani na Iran yatahakikisha kwamba Tehran inapata silaha za nyuklia, kitisho ambacho sio tu kwa mashariki ya kati lakini kwa dunia nzima.

Akiongea mbele ya bunge la Marekani, siku ya Jumanne bwana Netanyahu alisisitiza kwa wabunge hatari kubwa ambayo inaletwa na Iran yenye nyuklia kwa nchi yake.

“kama mashauriano yanayoendelea hivi sasa yanakubaliwa na Iran, makubaliano hayo hayataizuia Iran kutengeneza silaha za nyuklia-itairuhusu na kuhakikisha kwamba Iran itapata silaha hizo za nyuklia, nyingi tu, alisema Netanyahu”.

Iran inafadhili ugaidi duniani kote, alisema bwana Netanyahu akiongeza kwamba utawala wa Tehran una msimamo mkali , hauwezi kuaminiwa na makubaliano yanayofanyiwa kazi na Marekani hayatazuia azma ya Iran kutengeneza bomu, lakini pia inafungua njia ya kuelekea kwenye bomu”.

Benjamin Netanyahu
Benjamin Netanyahu

Bwana Netanyahu alisema ni vizuri kutokuwa na makubaliano kuliko kuwa na makubaliano ambayo ni mabaya. Haya ni makubaliano mabaya, mabaya sana. Ni bora tusiwe na makubaliano hayo”.

Bwana Netanyahu alipokelewa kwa shangwe na wabunge, wakati alipowasili kwenye ukumbi wa baraza la wawakilishi la Marekani, Jumanne. Haraka alijaribu kupunguza mvutano uliojitokeza wakati spika wa bunge John Boehner alipomualika Netanyahu kuzungumza bila ya kushauriana na White House.

XS
SM
MD
LG