Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 06, 2023 Local time: 19:45

Netanyahu atoa matamshi makali kwa Hezbollah


Magari yakionekana kuungua karibu na kijiji cha Ghajar kwenye mpaka wa Israel na Lebanon, Jan. 28, 2015.

Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu alisema jumatano kwamba wale waliohusika na shambulizi la kombora lililosababisha vifo kwenye msafara wa jeshi la Israel kwa maneno yake “watalipa gharama kamili”.

Majibizano ya makombora karibu na mpaka wa Syria na Lebanon yaliuwa wanajeshi wawili wa Israel na raia mmoja wa Spain mfanyakazi wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa huko kusini mwa Lebanon. Wanajeshi saba wa Israel pia walijeruhiwa.

Benjamin Netanyahu
Benjamin Netanyahu

Israel ilidai shambulizi hilo kufanywa na kundi la wanamgambo wa ki-Islam la Hezbollah lenye makao yake Lebanon. Bwana Netanyahu aliuambia mkutano wa baraza la mawaziri hapo jumatano kwamba Iran imekuwa ikiwatumia Hezbollah kujaribu kuweka “eneo jingine la kigaidi” kutoka eneo la Syria la Golan Heights.

Waziri mkuu huyo aliliambia baraza la mawaziri kuwa serikali ya Lebanon na utawala wa Rais wa Syria, Assad wanashirikiana majukumu ya matokeo ya mashambulizi kwa Israel ambayo yametokea kwenye maeneo yao.

Kwa mujibu wa walinda amani wa Umoja wa Mataifa makombora sita yalirushwa kwa Israel kutoka kijiji kimoja cha Lebanon na kusababisha Israel kujibu shambulizi. Makombora ya Hezbollah yalikuwa ya kulipiza kisasi kwa shambulizi moja la anga lililoshukiwa kufanywa na Israel kuelekea Syria mwanzoni mwa mwezi huu na kuuwa wanachama sita wa Hezbollah na Jenerali mmoja wa Iran.Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilikutana jumatano kuzungumzia hali hii.

Jen Psaki
Jen Psaki

Wakati huo huo msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Jen Psaki alisema Marekani inalaani vikali shambulizi la Hezbollah ikiliita ni ukiukaji wa sitisho la mapigano kati ya Israel na Lebanon. Psaki pia alisema Marekani inaunga uhalali wa Israel kujilinda yenyewe.

XS
SM
MD
LG