Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 11:09

Russia ilifuata sheria za kimataifa ilipoikaribia manowari ya Marekani


Rais wa Russia, Vladimir Putin akijibu maswali katika kipindi maalum cha kila mwaka mjini Moscow, April 14, 2016.
Rais wa Russia, Vladimir Putin akijibu maswali katika kipindi maalum cha kila mwaka mjini Moscow, April 14, 2016.

Russia inasema ndege zake za kijeshi zilifuata sheria zote za kimataifa ziliporuka karibu sana na manowari ya Marekani kwenye maji ya kimataifa katika bahari ya Baltic mapema wiki hii.

Wizara ya ulinzi ya Russia imesema leo kwamba ndege zake SU-24 zilikuwa zikifanya mazoezi ya kijeshi, Russia ilikuwa ikijibu ukosoaji wa Marekani, wizara hiyo imesema ndege hizo za Russia zilikaribia kabisa meli hiyo ya kivita ya USS Donald Cook na kurudi ikiwa imeheshimu hatua zote za usalama.

Taarifa hiyo ya wizara imesema manowari hiyo ya Marekani haikuwa mbali na eneo la kufanya operesheni kutoka kwenye kambi ya jeshi la Russia. Shirika la habari la Russia Tass linaeleza kwamba meli hiyo ilikuwa kilometa 70 kutoka kwenye kambi ya jeshi la majini la nchi hiyo.

XS
SM
MD
LG