Seneta wa Nakuru Susan Kihika amethibitisha kuwa watu watatu walikuwa ni waandishi wa habari katika timu yake ya kampeni.
Ndege hiyo ya kibinafsi yenye usajili 5Y NMJ ilizama katika ziwa Nakuru muda mfupi baada ya kupaa karibu na hoteli moja kuwachakua abiria fulani wanaoripotiwa kuwa wanasiasa.
Kufuatia kuzama huko maafisa wa idara ya kudhibiti majanga nchini Kenya wanaeleza kuwa bado hawajafahamu sehemu ndani ya Ziwa hilo ambako mabaki ya ndege hiyo yapo.
Abiria watano, wanaume wanne na mwanamke mmoja wanaoripotiwa kuwa katika ndege hiyo hawafahamiki iwapo bado wangali hai.
Shughuli za uokoaji kutoka vitengo vyote vya usalama nchini Kenya vimefika katika eneo la mkasa.