Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 03, 2023 Local time: 20:50

Ndege ya Ukraine yatunguliwa na kuuwa 49


wanaopigana kujitenga wakusanya silaha kutoka kwa ndege iliyotunguliwa

Wizara ya ulinzi inasema ndege hiyo ilikuwa ikikaribia kutua katika uwanja wa ndege wa Luhansk ilipopigwa risasi

Maafisa wa Ukraine wanasema watu wanaopigana kujitenga na kujiunga na Russia, wametungua ndege ya uchukuzi ya kijeshi na kuuwa watu wote 49 waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

Ofisi ya mwendesha mashataka mkuu huko Ukraine, ilisema wanajeshi 40 na wafanyakazi tisa waliuawa mapema leo Jumamosi baada ya ndege hiyo ya jeshi la angani la Ukraine kupigwa risasi na kuanguka.

Wizara ya ulinzi inasema ndege hiyo ilikuwa ikikaribia kutua katika uwanja wa ndege wa Luhansk ilipopigwa risasi.

Ukanda wa video unaonyesha mlipuko mkubwa karibu na uwanja huo wa ndege, unaoaminika kutoka kwa ndege hiyo.
XS
SM
MD
LG