Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 07:33

Ndege ya Ethiopian Airlines yaanguka, juhudi za kuitafuta zaendelea


Ndege ya Ethiopian Airlines Boeing 737-800
Ndege ya Ethiopian Airlines Boeing 737-800

Shirika la ndege la Ethiopia imesema kuwa ndege yake iliyokuwa inaondoka Addis Ababa, mji mkuu wa nchi hiyo ikiwa na abiria 149 na wafanyakazi wanane imeanguka na juhudi za kuitafuta ndege hiyo zinaendelea.

Shirika hilo limeposti ujumbe wa Twitter kuwa ndege hiyo nambari 302 iliruka majira ya saa 8:38 asubuhi kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole na kupoteza mawasiliano saa 8:44.

Ujumbe huo umeongeza kuwa juhudi za kuitafuta ndege hiyo na ukoaji zinaendelea na hadi sasa hakuna taarifa yeyote juu ya abiria na wafanyakazi hao waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

Waziri Mkuu Abiy Ahmed amesema katika ujumbe wake wa Twitter : “Ofisi ya Waziri Mkuu, kwa niaba ya serikali na watu wa Ethiopia, wanatoa rambirambi zao kwa familia za watu wote waliopoteza ndugu zao ambao walikuwa katika ndege hiyo ya Ethiopia Airlines 737 iliyokuwa katika safari zake za kawaida kuelekea Nairobi, Kenya Jumapili asubuhi.

Ujumbe wa Twitter

Office of the Prime Minister - Ethiopia @PMEthiopia

The Office of the PM, on behalf of the Government and people of Ethiopia, would like to express it’s deepest condolences to the families of those that have lost their loved ones on Ethiopian Airlines Boeing 737 on regular scheduled flight to Nairobi, Kenya this morning.

3,705

Twitter Ads info and privacy

4,933 people are talking about this

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG