Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 15:21

Ndege ya AirAsia yatoweka ikiwa na abiria 162


Ndege ya kampuni ya Airasia
Ndege ya kampuni ya Airasia

Kabla ya kupoteza mawasiliano na ndege hiyo, rubani wake alikuwa ameomba maafisa wanaongoza safari za ndege kumruhusu kupaa kilomita 1,800 ili kuepuka hali mbaya ya hewa.

Juhudi za kutafuta ndege ya AirAsia iliyokuwa na abiria 162 na wafanyakazi ,katika ziwa Java zimeahirishwa hadi Jumatatu asubuhi.

Ndege hiyo iliondoka mji wa Surabaya nchini Indonesia kuelekea Singapore iliporipotiwa kutoweka mwendo wa saa moja na dakika 24 nne asubuhi kwa saa za Indonesia, dakika 42 baada ya kuanza safari yake.

Indonesia inasema meli zake za uokozi zitabaki kwenye eneo hilo usiku kucha , lakini shughuli ya kuitafuta ndege hiyo kwenye maji hayo itarejelewa Jumatatu asubuhi.

Maafisa wanasema kabla ya kupoteza mawasiliano na ndege hiyo, rubani wake alikuwa ameomba maafisa wanaongoza safari za ndege kumruhusu kupaa kilomita 1,800 ili kuepuka hali mbaya ya hewa.

XS
SM
MD
LG