Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 14:14

Ndege ya EgyptAir yatua kwa dharura ikihofia bomu


Ndege moja ya abiria ya shirika la ndege la Egyptair, ambayo ilikuwa ikielekea mjini Beijing, ilitua kwa dharura nchini Uzbekistan mapema leo.

Maafisa wa Misri wamesema tishio la uwongo kwamba mlikuwa na bomu kwenye ndege hiyo, ndilo lilisababisha kutua huko kwa ghafla, kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Urgench.

Abiria waliondolewa kwa ndege hiyo, lakini wakati upekuzi ulipofanywa, hakuna vilipuzi vyovyote vilivyopatikana.

Afisa mmoja wa Misri alisema kwamba ndege hiyo ilikuwa inatayarishwa ili kuendelea na safari, na kwamba tishio hilo lilikuwa la mzaha tu.

Ndege hiyo nambari MS955, ilikuwa inatoka Cairo, ilikuwa na abiria 118 na wahudumu 17. Katika siku za hivi karibuni, ndege za Egyptair zimekuwa zikipata tishio za mzaha za mabomu, tangu ndege yake iliyokuwa ikitoka Paris kwelekea Cairo, ilipoanguka kwenye bahari ya Mediterranean mwezi jana.

Uchunguzi bado unaendelea kubaini kilichosabisha ndege hiyo aina ya Airbus 320, kupoteza mawasiliano ya radar mnamo tarehe 19 mwezi Mei, na kuanguka baharini, huku ikiwaua watu wote 66 waliokuwemo.

XS
SM
MD
LG