Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 22, 2023 Local time: 18:44

Nchi zilizoendelea zagombea usambazaji wa nishati


Vituo vya kujaza mafuta viliishiwa katika miji ya Uingereza.

Kuanzia Marekani  hadi Ujerumani, nchi zilizoendelea zinagombania kupata usambazaji wa nishati na kukidhi mahitaji ya watumiaji yanayoongezeka ya bidhaa.

Kuanzia Marekani hadi Ujerumani, nchi zilizoendelea zinagombania kupata usambazaji wa nishati na kukidhi mahitaji ya watumiaji yanayoongezeka ya bidhaa. Minyororo ya ugavi iliyovurugwa na janga la COVID-19 inahangaika kukabiliana na viwanda haviwezi kukidhi mahitaji ya wateja, ambao wanatumia zaidi ya kawaida, matokeo ya serikali kuingiza dola trilioni 10 kwa pamoja katika uchumi wao, wanasema wachambuzi wa biashara.

Uhaba nchini Uingereza umechukua vichwa vya habari huku wanunuzi wakikumbana na makabati matupu ya chakula huku matunda na mboga mboga hazipatikani. Wakuu wa maduka makubwa walionya Jumatano kuwa huenda wakalazimika kupunguza nyama ili kuzuia ununuzi wa hofu, haswa wakati wa kuelekea Krismasi.

Changamoto za usambazaji Uingereza zimeongezeka kutokana na kuondoka kwake kutoka Umoja wa Ulaya, mshirika wake mkuu wa kibiashara. Lakini majirani wa Ulaya pamoja na Marekani, pia wanaripoti uhaba wa nguo na bidhaa za kielektroniki. Watengenezaji wanasema wanapata shida kupata microchips kwa sababu ya kusimamishwa kwa kiwanda huko Asia.

XS
SM
MD
LG