Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 20:02

Nchi za Kiarabu zataka suluhisho la haraka kwa mzozo wa Sudan


Rais wa Sudan Omar al-Bashir (L)mwenye kilemba cheupe na Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir(R) kwenye uwanja wa ndege wa Khartoum
Rais wa Sudan Omar al-Bashir (L)mwenye kilemba cheupe na Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir(R) kwenye uwanja wa ndege wa Khartoum

Rais wa Sudan Omar al-Bashir anasema Sudan Kusini inawasaidia waasi na kwamba serikali yake haitakaa kimya kwa hilo

Umoja wa nchi za Kiarabu umeungana na nchi nyingine kuisihi Sudan kuruhusu misaada ya kibinadamu ipelekwe kwa raia wa Sudan Kusini katika mikoa ya Kordofan na Blue Nile ambapo wafanyakazi wa kutoa misaada wanasema watu wapatao 14,000 wanahitaji msaada wa dharura wa chakula.

Maafisa wa Marekani wanaamini makubaliano ya kuruhusu misaada ya chakula yatasaidia kutatua baadhi ya mizozo ya mpaka na uhasama kati ya Sudan na Sudan Kusini. Lakini kuna tatizo la uasi unaoendelea katika mkoa wa Kordofan Kusini.

Wapiganaji katika milima ya Nuba hawakuruhusiwa kujitenga na Sudan wakati Sudan Kusini ilipotangaza rasmi uhuru wake mwezi Julai mwaka jana. Kwa hiyo bado wanapigana na jeshi la Sudan- SAF.

Rais wa Sudan Omar al-Bashir anasema Sudan Kusini inawasaidia waasi na kwamba serikali yake haitakaa kimya wakati serikali mpya ya Juba ikiendelea kutishia usalama wa taifa lake. Naye Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir anasema Khartoum tayari inaunga mkono mashambulizi ya kijeshi katika nchi yake.

Kufuatia mvutano huo jumuiya ya nchi za Kiarabu sasa imeungana na Umoja wa Mataifa kuisihi Khartoum kuruhusu mashirika ya kimataifa ya kutoa misaada kuingia mikoa ya Kordofan na Blue Nile.

Mashirika hayo yanasema hali ya kibinadamu inazidi kuzorota Sudan Kusini na kwenye mpaka wake na Khartoum na kwamba maeneo ya mpakani ya Kordofan kusini na Blue Nile yamedumazwa zaidi na ongezeko la bei ya vyakula, mafuta pamoja na mtafaruku unaoendelea. Yanasema katika siku za karibuni itakuwa vigumu kupeleka misaada katika maeneo hayo kwa sababu mvua zinategemewa kunyesha na barabara nyingi hazitapitika tena.


XS
SM
MD
LG