Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 08:44

NATO yasema haitapunguza mashambulizi Libya


Ndege za kijeshi za NATO.
Ndege za kijeshi za NATO.

Kamanda wa NATO asema mashambulizi yataendelea Libya kuiwekea shinikizo serikali ya Gadhafi.

Kamanda wa NATO wa operesheni ya Libya anasema majeshi ya muungano hayapunguzi mashambulizi ya anga licha ya wito wa baadhi ya mataifa kusimamisha operesheni hiyo.

Luteni Jenerali wa Canada Charles Bouchard amesema operesheni hiyo inayoingia mwezi wa nne imepata maendeleo makubwa na kwamba mashambulizi dhidi ya raia na serikali ya Libya yamepungua.

Maelezo ya NATO yamekuja wakati mwendesha mashitaka wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu akiwataka wasaidizi wa Moammar Gadhafi wamkamate na wamfikishe kwenye mahakama hiyo kujibu kesi.

Maelezo hayo ya Luis Moreno Ocampo hii leo yamekuja baada ya mahakama iliyoko The Hague kutoa hati jana ya kukamatwa kwa Bw.Gadhafi na wasaidizi wake wakuu wawili kwa makosa ya uhalifu wa kivita yanayohusiana na kukandamizwa kwa uasi wa upinzani.

XS
SM
MD
LG