Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 03:52

Nato yaongeza mashambulizi Tripoli


Moja ya majengo yalioharibiwa na mashambulizi ya anga ya Nato huko Libya. (AP Photo/Darko Bandic)
Moja ya majengo yalioharibiwa na mashambulizi ya anga ya Nato huko Libya. (AP Photo/Darko Bandic)

Mashahidi wanasema walisikia milipuko na kuona moshi ukifuka kwenye bandari ya mji huo ikiwa ni kuongezeka kwa mashambulizi ya NATO.

NATO imefanya mashambulizi zaidi katika mji mkuu wa Libya, Tripoli katika jaribio la kuyazuia majeshi yanayomuunga mkono Moammar Gadhafi.

Mashahidi wanasema walisikia milipuko na kuona moshi ukifuka alhamisi usiku kutoka kwenye Bandari ya mji huo.

Wakati huo huo katika maeneo mengine majeshi ya serikali yalishambulia wapiganaji wa upinzani katika mji wa mlimani kusini magharibi mwa Tripoli. Pande hizo mbili zimeonekana zikijaribu kuchukua udhibiti wa barabara ambayo inakwenda kwenye mji mkuu ngome kuu ya BW. Gadhaffi.

Kiongozi wa Libya alijitokeza kwa muda mfupi katika televisheni ya taifa Alhamisi usiku akionekana kwa mara ya kwanza tangu wiki iliyopita.

XS
SM
MD
LG