Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:59

NATO Yagomea Hoja ya Gadhafi


Wapiganaji waasi wakitafuta wafuasi wa Gadhafi katika mji wa Misrata hivi karibuni
Wapiganaji waasi wakitafuta wafuasi wa Gadhafi katika mji wa Misrata hivi karibuni

Afisa wa NATO asema wanataka kuona vitendo kutoka kwa kiongozi huyo wa Libya sio maneno matupu

NATO imegomea hoja ya kiongozi wa Libya Muammar Gadhafi kutaka mazungumzo ili kumaliza mgogoro wa Libya.

Afisa mmoja wa NATO alisema Jumamosi ushirika huo wa kujihami unataka kuona vitendo sio maneno matupu kutoka kwa kiongozi huyo wa Libya. Alisema NATO itaendelea na operesheni zake Libya kadiri ambavyo maisha ya raia wa nchi hiyo yanatishiwa.

Waasi wa Libya pia wamegomea hoja ya Gadhafi ya mazungumzo wakisema muda wa mapatano umepita. Waasi kutoka baraza la utawala wa mpito wamesema serikali ya Gadhafi imepoteza uaminifu kabisa.

Mapema Jumamosi, Gadhafi alisema katika hotuba ya televisheni kuwa yuko tayari kwa mazungumzo kama NATO itaawacha kushambulia serikali yake, lakini alisema hana mpango wa kujiuzulu.

XS
SM
MD
LG