Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 13:56

NATO yachunguza madai ya Libya


Madaktari wa Libya wakionyesha maiti za mtu mmoja na mtoto zilizokutwa katika nyumba inayosemekana ilishambuliwa na NATO Jumapil 19, 2011 mjini Tripoli.

NATO yakiri ilifanya shambulizi jumamosi usiku lakini inasema mashambulizi yake yanalenga maeneo ya kijeshi

Maafisa wa NATO wanasema watachunguza madai ya serikali ya Libya kuwa raia saba wameuawa katika shambulizi la anga ndani ya mji wa Tripoli mapema Jumapili.

Serikali ilionyesha nyumba moja iliyokuwa imeharibiwa vibaya katika eneo la Souq al Juma, eneo ambalo ni la makazi ya raia katika mji mkuu Tripoli.

Maiti mbili zilionekana zikitolewa katika kifusi. Maiti nyingine tatu, ikiwa ni pamoja na watoto wawili, ilionyeshwa katika hospitali moja ya mjini humo. Msemaji wa serikali ya Libya Moussa Ibrahim alizungumza na waandishi wa habari wa kigeni waliopelekwa kwenye eneo la tukio.

"Kimsingi, huu ni usiku mwingine wa mauaji na udhalilishaji unaofanywa na NATO dhidi ya Tripoli," alisema Ibrahim. "Mmeona kwa macho yenu wenyewe maafa yanayotokea kila siku Tripoli."

NATO inakiri kuwa ilifanya mashambulizi usiku wa kuamkia Jumapili katika mji huo mkuu wa Libya, kama sehemu ya amri ya Umoja wa Mataifa kuhakikisha ukanda wa kutorusha ndege ili kulinda maisha ya raia. Lakini ushirika huo wa kujihami wa Ulaya unasema unapiga tu maeneo ya kijeshi mjini Tripoli.

XS
SM
MD
LG