Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 12:10

NATO itaendeleza operesheni za kijeshi nchini Libya


Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Ahmet Davutoglu
Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Ahmet Davutoglu

Arab League, Morocco na utawala wa Palestina wathibitisha kuunga mkono upinzani wa Libya.

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki anasema NATO itaendelea na operesheni za kijeshi huko Libya mpaka usalama utakaporejea. Ahadi hiyo imekuja wakati mapigano yakiendelea katika mji mkuu wa Libya, Tripoli na wakati viongozi wa dunia wakimhimiza kiongozi wa Libya, Moammar Gadhafi kuachia madaraka.

Ahmet Davutoglu aliwaambia waandishi wa habari Jumanne katika ngome ya waasi huko Benghazi kwamba mali za rais wa Libya zilizozuiwa lazima zikabidhiwe kwa watu wa Libya ambao wanahitaji sana hizo rasilimali. Pia alirejea kuelezea uungaji mkono wa Uturuki kwa baraza la taifa la mpito huku waasi wakiendelea kupigana kupata udhibiti wa ngome ya Gadhafi ya Tripoli.

Arab League , utawala wa Palestina na Morrocco pia walithibitisha kuunga mkono upinzani. Shirika la habari la taifa la Morocco MAP lilisema waziri wa mambo ya nje Taib Fass Fihiri atasafiri kwenda Benghazi Jumanne.

XS
SM
MD
LG