Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 20:34

Nana Akufo-Addo ashinda awamu ya pili ya urais Ghana


Rais Nana Akufo-Addo akiwasilimia wafuasi wake katika kituo cha kupigia kura huko Kyebi, Ghana, Dec. 7, 2020.
Rais Nana Akufo-Addo akiwasilimia wafuasi wake katika kituo cha kupigia kura huko Kyebi, Ghana, Dec. 7, 2020.

Wafuasi wa Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo wamekusanyika nje ya makazi yake kusherehekea kuchaguliwa kwake tena kwa muhula wa pili, baada ya uchaguzi wa rais uliokuwa na upinzani mkali.

Akufo-Addo wa chama chenye mrengo wa kati kulia cha New Patriotic Party (NPP) alipata kura 6,730,413 au asilimia 51.59 ya kura wakati John Mahama wa chama chenye mrengo wa kati kushoto cha National Democratic Congress (NDC) alipata 6,214,889 sawa na asilimia 47.36, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jean Adukwei Mensa alisema.

Matokeo ya kura ya Jumatatu yalikuja saa kadhaa baada ya polisi kusema watu watano wameuwawa katika ghasia zinazohusiana na uchaguzi, wakiweka doa katika ya nchi inayosifiwa kwa demokrasia thabiti.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Ghana Jean Mensa alitangaza kuwa Rais Nana Akufo-Addo ameshinda muhula wa pili baada ya uchaguzi wa rais uliokuwa na upinzani mkali, akimshinda mpinzani wake wa muda mrefu John Mahama.

“Mwisho wa upigaji kura, Nana Addo Dankwa Akufo-Addo wa New Patriotic Party, alipata kura 6,730,413, ikiwa ni asilimia 51.595 ya kura halali zilizopigwa."alisema Mensa.

Waangalizi waliona upigaji kura ukiwa huru na wa haki kwa ujumla lakini hali ya kisiasa ilizorota Jumanne wakati Mahama alimshutumu mpinzani wake kwa kuonyesha hati ambazo hazina demokrasia.

Siku ya Jumanne, Mahama alimshtumu Akufo-Addo kwa kutumia jeshi kwa nia ya kushawishi matokeo, madai ambayo serikali ilisema ni ya uwongo.

“Huwezi kutumia jeshi kujaribu kubadili baadhi ya matokeo katika maeneo bunge ambayo tumeshinda. Tutapinga majaribio yoyote ya kupindua mapenzi huru ya watu wa Ghana.” Alisema Mahama.

Ghana imekuwa na mabadiliko saba ya madaraka kwa njia ya amani tangu kurudi kwa demokrasia zaidi ya miaka 30 iliyopita, kwani malalamiko ya baada ya uchaguzi yamekuwa yakishughulikiwa kupitia mahakama jambo la nadra katika eneo lenye changamoto.

Mwangalizi mkuu wa Jumuiya ya Ulaya, Javier Nart, aliambia mkutano na waandishi wa habari Jumatano kwamba "Waghana walipiga kura kwa uhuru.

Waghana walijitokeza kwa wingi kupiga kura

Licha ya janga la corona, idadi ya waliojitokeza ilikuwa kubwa Jumatatu, na watu 13,434,574 walipiga kura ikiwa ni asilimia 79 ya wapiga kura waliojiandikisha. Akufo-Addo na Mahama siku ya Ijumaa walikuwa wametia saini mkataba wa amani wa ishara, wakati umoja wa mataifa 15 wa nchi za ECOWAS ulihimiza vyama vyote vya kisiasa na uongozi wao kuheshimu.

Ghana imerekodi ukuaji wa hali ya juu wakati wa kipindi cha kwanza cha Akufo-Addo madarakani wakati alifanya kazi kuubadilisha uchumi unaotegemea sana uuzaji nje wa kakao na hivi karibuni mafuta na dhahabu.

Lakini wakati Ghana imepiga hatua kubwa, wengi bado wanaishi katika umaskini uliokithiri na upatikanaji mdogo wa maji safi au umeme.

Wakiwa wameathiriwa sana na janga ukuaji katika taifa la watu milioni 30 unatarajiwa kushuka mwaka huu hadi chini kabisa katika miongo mitatu, hadi asilimia 0.9 kulingana na Shirika la Fedha la Kimataifa, ikiwa ni kupungua kwa kasi kutoka ukuaji wa asilimia 6.5 mnamo mwaka 2019.

Imetayarishwa na Sunday Shomari , VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG