Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 14:02

Namibia yafurahishwa na juhudi za Zimbabwe


Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe (L) akipeana mikono na Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai, Harare, May 22, 2013.
Waziri wa mambo ya nje wa Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah alisema serikali yake imetiwa moyo na uamuzi wa viongozi wa Zimbabwe wa kutatua tofauti zao wakati nchi hiyo ikiwa inaelekea kwenye uchaguzi mkuu.

Bibi, Netumbo Nandi-Ndaitwah anasema serikali ya Windhoek inashirikiana na jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika-SADC kama sehemu ya juhudi za kuisaidia Zimbabwe ipige kura kwa amani.

Matamshi yake yamekuja baada ya Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe na mpinzani wake Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai walipokubaliana juu ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Julai 31.

Anasema Windhoek na Harare wataendelea kufurahia diplomasia tulivu na mahusiano yao mazuri. Katika masuala mengine, Nandi-Ndaitwah alisema Namibia ilishirikiana na nchi jirani pamoja na Umoja wa Afrika kusaidia kuhakikisha amani na uthabiti barani humo.

Alisema serikali yake inaunga mkono juhudi za kimataifa za kutatua changamoto za usalama katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC. “Namibia kama mwanachama wa SADC kwenye ulinzi na usalama kila siku inafuatilia kazi za usalama katika eneo, na kwamba hivi ndio namna tunavyofanya majukumu yetu kama mwanachama wa eneo hili”, alisema Nandi-Ndaitwah.

Wakati huo huo Namibia inatarajiwa kuchukua uenyekiti wa taasisi hiyo ya kieneo katika siasa, ulinzi na usalama wakati viongozi wa kieneo wa SADC wanapanga kukutana katika mkutano wa kipekee mwezi Agosti.
XS
SM
MD
LG