Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 06, 2023 Local time: 07:01

Namibia inakaribia kuwa na rais mwanamke wa Kwanza


Naibu wa rais wa chama cha Swapo Netumbo Nandi-Ndaitwah baada ya kutangazwa mshindi Nov. 29, 2022. (Vitalio Angula/VOA)

Chama kinachotawala nchini Namibia kimemteua Netumbo Nandi-Ndaitwah kama makam rais wake na hivyo kumueka katika nafasi nzuri ya kuwa mgombea wa urais wa kwanza mwanamke nchini humo, katika uchaguzi wa mwaka 2024 wakati rais wa nchi hiyo atakapostaafu.

Netumbo Nandi Ndaitwah ni naibu waziri mkuu katika serikali ya sasa, na uteuzi wake katika nafasi ya juu ya chama cha Swapo, umefanyika wakati wa kongamano kuu la chama.

Kulingana na katiba ya chama cha SWAPO, Nandi Ndaitwah atakuwa mgombea wake wa urais wakati rais wa sasa Hage Geingob atakapomaliza mihula yake miwili madarakani, ambayo imesalia miezi 15.

Ndaitwah amewashinda wagombea wengine wawili akiwemo waziri mkuu wa sasa katika uchaguzi uliohusisha wanachama wa ngazi ya juu 700 na kuhudhuriwa pia na viongozi wa chama kinachotawala nchini Zimbabwe, ZANU-PF.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG