Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 12:26

Kiswahili Chapata Pigo Kwa Kifo cha Nabhany


Prof. Sheikh Ahmed Nabhany
Prof. Sheikh Ahmed Nabhany

Wanazuoni wa Kenya na wengine wengi katika Afrika Mashariki wametoa rambi rambi zao kwa familia ya Sheikh Ahmed Mohamed Nabhany, ambaye aliaga dunia Alhamisi huko kijijini kwake alikozaliwa, Matondoni, Lamu nchini Kenya.

Profesa Nabhany si mgeni katika tasnia ya Kiswahili. Amekuwa mstari wa mbele kukuza na kuendeleza lugha pamoja na kueneza matumizi bora ya lugha hiyo, ambayo imezidi kuenziwa na wengi katika ukanda wa Afrika Mashariki na kote ulimwenguni.

Profesa alizaliwa tarehe 27 Novemba 1927 huko Lamu na baadaye kuhamia mjini Mombasa kwa shughuli za kikazi.

Professa amezikwa Alhamisi katika makaburi ya Matondoni Magharibi ya Lamu. Na amemwacha mjane na watoto watatu.

Mazishi ya Profesa Nabhany
Mazishi ya Profesa Nabhany

Kabla kufariki alikuwa katika matibabu na kulazwa hospitalini huko kijijini kwake Matondoni, kisiwani Lamu.

Mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili VOA ameripoti kuwa lugha ya Kiswahili inayokua kwa kasi zaidi kote ulimwenguni leo imepata pigo kubwa baada ya kufariki kwa moja wa wataalam na walezi wake huko nchini Kenya.

Ameeleza kuwa alikuwa mstari wa mbele katika kukuza na kuiendeleza lugha pamoja na kueneza matumizi bora ya lugha hii ambayo imezidi kuwavutia wengi katika ukanda wa Afrika Mashariki na kote ulimwenguni.

Henry Indindi, Mtaalam wa Lugha ya Kiswahili na Mwandishi wa vitabu amekuwa akifuata nyayo za Profesa.

Kwa mujibu wa Bwana Indindi, Profesa Nabhany amekuwa mtunzi stadi wa mashairi ambayo yamempa hadhi kubwa kote nchini.

Naye Professa Ken Walibora, mwanahabari na mwandishi maarufu ulimwenguni anasema amezipokea taarifa za kifo cha Profesa Nabhany kwa mshtuko na masikitiko mkubwa mno.

Vile vile Profesa Walibora anaelezea kuwa Nabhany amekuwa mtu wa kupigiwa mfano katika uundaji wa misamiati na istilahi za lugha adhimu ya Kiswahili.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Kennedy Wandera, Kenya

XS
SM
MD
LG