Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 23:01

Mzozo wazidi kunukia Guinea Bissau


Askari akiwa katika lindo karibu na jengo la bunge Guinea Bissau
Askari akiwa katika lindo karibu na jengo la bunge Guinea Bissau

Vyama vya upinzani vyakataa pendekezo la viongozi wa mapinduzi

Kundi la vyama vya siasa nchini Guinea Bissau limetupilia mbali pendekezo la jeshi linalohusika na mapinduzi ya wiki hii kuunda serikali ya mpito mpaka pale uchaguzi wa urais utakapofanyika .

Vyama hivyo vilikutana na jeshi jumanne na mazungumzo zaidi yanatarajiwa kufanyika jumapili. Vyama vya siasa vinataka suluhisho linalotokana na katiba ya nchi.

Jeshi lilichukua udhibiti alhamisi na kuvuruga kampeni za uchaguzi na kutumbukiza taifa hilo la magharibi katika ghasia mpya.

Uongozi wa jeshi ulimkamata mgombea aliye mstari wa mbele wa kiti cha urais na waziri mkuu wa zamani Carlos Gomes Junior pamoja na rais wa mpito Raimundo Pereira na kuwatia jela baada ya kuvamia nyumba zao.

jumuiya za kimataifa zimeshutumu vikali mapinduzi hayo ya kijeshi katika taifa hilo la magharibi ambalo april 29 lilitarajiwa kufanya uchaguzi wa marudio. Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban ki- Moon na baraza la usalama la umoja wa mataifa walitoa taarifa kama hiyo.

XS
SM
MD
LG