Wanawake watatu wameuawa nchini Somalia wiki iliyopita kwa kile polisi wanasema kinatokana na ugomvi wa nyumbani. Bunge la nchi hiyo limetoa wito wa uchunguzi wa haraka na kuwakamata watuhumiwa wakati raia wakieleza hasira zao.
Mauaji hayo yametokea Mogadishu, mkoa wa Lower Shabelle na wilaya ya Qoryooley. Mwanamke mmoja alichomwa kisu, na wa pili alipigwa risasi na wa tatu alichomwa moto, waume zao walishutumiwa kuhusika na mauaji hayo.
Mkuu wa Polisi Moalim Mahdi, mkuu wa mkoa wa Banadir inajumuisha Mogadishu, ameahidi hatua zichukuliwe dhidi ya watuhumiwa.
Mkuu wa polisi wa mkoa wa Banadir Moalim Mahdi ambayo unajumuisha mji mkuu wa Mogadishu ameahidi kuchukua hatua dhidi ya watenda maovu hayo.
Aina mbalimbali za unyanyasaji wa kijinsia zimeenea Somalia. Hali ambayo inasababishwa na kutokuwepo kwa mfumo wa sheria kuzuia unyanyasaji wa aina hiyo.
Mkurugenzi wa kundi la kutetea haki za wanawake na watoto nchini Somalia Amina Haji Elmi, amesema wanawake wa Somalia” pamoja na raia wengine wamekuwa wakiishi katika nchi iliyoharibiwa na vita.
Mwaka 2020, bunge lilijadili mswaada uliokua na utata kukabiliana na unyanyasaji kwa misingi ya ngono lakini lililazimika kusitisha majadiliano kufuatia shinikizo kutoka ndani na nje ya nchi kuhusiana na kifungu kimoja kinachoruhusu ndoa za utotoni, ndoa za kulazimisha na ukiukaji wa haki za wanawake
Forum