Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 13:36

Mzozo wa Rwanda na DRC, pamoja na makundi ya uasi yatishia sokwe wa Virunga


Sokwe wa hifadhi ya milima ya Virunga.
Sokwe wa hifadhi ya milima ya Virunga.

Mivutano kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda inatishia sokwe wa milimani walio hatarini kutoweka.

Licha ya matatizo hayo, jamii zinazoishi pande zote mbili za mpaka zimeungana ili kuboresha uhifadhi wa sokwe.

Jospin Muibonge anasomea utalii na uhifadhi katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Teknolojia Mpya huko Goma, mji ulioko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwenye mpaka wa Rwanda.

Amevuka hadi wilaya ya Musanze nchini Rwanda ili kujifunza zaidi kuhusu uhifadhi wa kijamii kutoka kwa shirika lisilo la kiserikali liitwalo Red Rocks Initiative for Sustainable Development.

Anasema lengo lake ni kuzisaidia jamii za wenyeji nchini DRC kufaidika na utalii wa hifadhi.

"Ninajifunza hapa ili kujaribu tu kunakili vitu wanavyofanya hapa, wanafanya nini ili kiweze kunakiliwa Kongo , katika nchi yangu.”

DRC na Rwanda, pamoja na Uganda, zinaunganishwa na Milima ya Virunga, kwenye milima ya volkano nane ambayo ni makazi ya zaidi ya nusu ya sokwe wa milimani waliosalia duniani.

Katika milima upande wa DRC, Mbuga ya Taifa ya Virunga haijafikiwa kwa angalau miezi tisa kutokana na harakati za makundi ya waasi katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa taarifa za shirika la African Wildlife Foundation, milima ya volcano na viumbe vinavyo ishi katika mbuga hiyo vilijumuishwa kwenye orodha ya urithi wa dunia wa UNESCO mwaka 1979.

Lakini ukosefu wa usalama wa kisiasa, ujangili na uchimbaji wa madini umeishusha hadhi hifadhi hiyo kuwa ya Urithi wa Dunia ulio hatarini, ambapo hifadhi hiyo ilisalia tangu 1994.

David Nenwa ni mhudumu wa watalii huko Goma na anasema shughuli za hivi karibuni za vikundi vya waasi katika eneo hilo zimetishia zaidi mbuga hiyo na jamii zinazowategemea.

“Hali ya Virunga si nzuri, na hivyo hatupeleki watalii huko kwa sababu ya hali hiyo. Ni vita, kwa sasa. Labda wakati amani itakaporejea tena, tutajaribu kupeleka watu huko."

Ili kusaidia, Juhudi za Red Rocks nchini Rwanda zinasaidia jamii katika pande zote za milima kushiriki kujipatia ujuzi katika sanaa, ufundi na shughuli za utalii za kijamii.

Kulingana na Mkurugenzi Mtendaji wa mpango huo, Greg Bakunzi, kuwalinda sokwe ni jukumu la jamii zinazoishi kuzunguka milima hiyo.

“Kuwa na hifadhi ya taifa inayo husisha nchi tatu, siku zote naona ni jambo muhimu, kwa sababu sokwe hawajui mipaka, hivyo wanazunguka kwa uhuru. Tunachotaka kufanya, ni kuhakikisha tulichofanya kwa upande wa Rwanda pia tunashirikishwa.”

Anasema mradi huo unalenga wanawake na vijana wanaoishi katika mazingira magumu kutoka Rwanda na Kongo kwa kuwasaidia kutengeneza kipato mbadala kupitia miradi endelevu na mipango ya utalii.

XS
SM
MD
LG