Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 02:28

Mzozo wa Ethiopia umesababisha ukosefu wa chakula Tigray


Mzozo wa chakula waongezeka Tigray. (AP Photo/Ben Curtis, File).
Mzozo wa chakula waongezeka Tigray. (AP Photo/Ben Curtis, File).

Mzozo uliodumu kwa takriban miaka miwili nchini Ethiopia umesabaisha ukosefu wa chakula kwa wakaazi wa Tigray na makundi ya misaada yanataabika kufika katika maeneo ya mbali kutokana na ukosefu wa mafuta, shirika la  mpango wa chakula ulimwenguni limesema Ijumaa.

Katika tathmini yake WFP imesema licha ya kwamba usambazaji wa misaada umeanza tena baada ya serikali kuu kutangaza sitisho la mapigano mwezi March, kiwango cha utapiamlo kimeongezeka sana na kinatarajiwa kuwa kibaya zaidi .

Huduma kama za kibenki na za mawasiliano ya simu zimefutwa katika mkoa wa Tigray ambako kuna zaidi ya wakazi milioni 5.5, siku kadhaa baada ya jeshi la taifa na washirika wake kuondoka mwaka mmoja uliopita.

Bado huduma hizo hazijarejeshwa , hali inayowazuiya watu kununua chakula WFP imesema. Ripoti hiyo imesema njaa na utapiamlo vimeongezeka sana na hali imezidi kuwa mbaya wakati watu wanaelekea katika kipindi cha mavuno mwezi Octoba mwaka huu.

Nusu ya wanawake wajawazito au wanaonyonyesha huko Tigray wana utapiamlo pamoja na theluthi moja ya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano na kusababisha kudumaa na vifo wakati wa kujifungua , ripoti hiyo imegundua.

XS
SM
MD
LG