Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 07:30

Mwili wa mwanafunzi kutoka Zambia aliyekufa akipigania Russia nchini Ukraine umerudishwa nyumbani


Gari lililobeba mwili wa mwanafunzi wa Zambia Lemekhani Nyireda ulipowasili katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Kenneth Kaunda, Lusaka, Zambia Dec 11, 2022
Gari lililobeba mwili wa mwanafunzi wa Zambia Lemekhani Nyireda ulipowasili katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Kenneth Kaunda, Lusaka, Zambia Dec 11, 2022

Mwili wa mwanafunzi mwenye umri wa miaka 23 raia wa Zambia, aliyefariki dunia katika vita nchini Ukraine, umerejeshwa nyumbani nchini Zambia.

Mwili wa Lemekani Nyirenda, ambaye alikuwa anasomea uhandisi kuhusu nyuklia, nchini Russia kabla ya kujiunga na jeshi, umefikishwa nyumbani na kupokelewa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kenneth Kaunda, mjini Lusaka, jana Jumapili.

Japo alikuwa mwanafunzi ambaye alikwenda Russia kwa ufadhili wa elimu ya juu, Lemekani alihukumiwa kifungo cha miaka 9 jela kwa makosa ya ulanguzi wa dawa za kulevya mnamo Aprili mwaka 2020.

Alisamehemewa baadaye kupitia mpango maalum wa serikali wa kutoa msamaha kwa masharti kwamba angekubali kushiriki katika vita nchini Ukraine, na aliuwawa akiwa katika mapigano.

Waziri wa mambo ya nje wa Zambia Stanley Kakubo amesema kwamba serikali ya Zambia imeiomba Russia kutoa maelezo zaidi kuhusiana na kifo cha Lemekani.

XS
SM
MD
LG