Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 23, 2025 Local time: 10:07

Waislamu duniani waanza ibada ya Ramadhan


Mwezi mtukufu wa Ramadhan umeanza hii leo ambapo mamilioni ya Waislam duniani kote wanafunga.

Mwaka huu nchi za upande wa kaskazini mwa dunia umeingia katika kipindi cha kiangazi ambapo inakuwa ni siku ndefu zaidi katika mwaka na kupelekea kipindi kirefu cha kufunga katika kipindi cha mzunguko wa mwezi kwa mujibu wa jarida la 'The Week.'

Baadhi ya Waislam watakuwa wakifunga kuufikia saa 17 kwa siku.

Dr. Razeen kutoka Chuo Kikuu cha Oxford anaonya watu wasile sana wakati wa kufuturu kwa ajili ya afya zao kwa mujibu wa jarida la afya la Uingereza NHS.

XS
SM
MD
LG