Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 18:47

Mwenge wa Olimpiki waanza safari ya Brazil


Mwanamke akiwasha mwenge wa Olimpiki wakati wa sherehe za kuwasha mwenge huko Ancient Olympia, Ugiriki April 21, 2016.
Mwanamke akiwasha mwenge wa Olimpiki wakati wa sherehe za kuwasha mwenge huko Ancient Olympia, Ugiriki April 21, 2016.

Mwenge wa Olimpik umeanza safari ya Rio De Janeiro kwa michuano ya Olimpiki mwezi Agosti.

Mwenge huo uliwashwa katika hafla Alhamisi huko Olympia, Ugiriki eneo ilikoanzishwa michuano ya Olimpiki.

Watu wapatao 450 watabeba mwenge huo katika mbio za siku 6 nchi nzima ya Ugiriki ikiwa ni pamoja na mkimbizi wa Syria ambaye ameomba hifadhi katika nchi hiyo.

Mwenge huo baadaye utawasili katika nchi mwenyeji wa michuano hiyo Brazil na kuanza mbio zake Mei 3. Mwenge huo utapita katika miji 83 ya Brazil na vitongoji 500 huku ukibebwa na watu 12,000.

XS
SM
MD
LG