Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 23:12

Mwendesha Mashtaka wa ICC anafanya uchunguzi wa  dharura kwa tuhuma za uhalifu wa kivita katika mji wa al-Fashir

Mtu mmoja akitembea na mabakuli ya chakula wakati familia za wasudan zikisaidia watu waliopoteza makazi yao Juni 3, 2024.
Mtu mmoja akitembea na mabakuli ya chakula wakati familia za wasudan zikisaidia watu waliopoteza makazi yao Juni 3, 2024.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC anafanya uchunguzi wa  dharura kwa tuhuma za uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu katika mji wa al-Fashir  huko Darfur ambao umekuwa uwanja mpya wa mapambano  kati ya jeshi la Sudan na Kikosi cha RSF.

Katika taarifa ya video iliyotolewa leo Jumanne, mwendesha mashtaka Karim Khan alisema ICC inafanya uchunguzi wa kina kuhusu uhalifu wa kinyama unaowezekana kufanywa hivi sasa huko Darfur.

"Nina wasiwasi mkubwa kuhusu shutuma za kusambaa uhalifu wa kimataifa unaofanywa huko al-Fashir na maeneo yanayoizunguka, kama tunavyozungumza," Khan alisema, akiongeza kuwa ofisi yake inachunguza tuhuma hizo kwa uharaka.

Wachunguzi wake wameona kuna shutuma za kuaminika kwa kile kilichoonekana kama mashambulizi ya kikabila dhidi ya raia, ubakaji mkubwa na mashambulizi dhidi ya hospitali, aliongeza.

Forum

XS
SM
MD
LG