Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 20:01

Muasisi wa kundi la Wagner huenda ni miongoni mwa abiria walofariki kwenye ajali ya ndege


Mkuu wa kundi la mamluki la Wagner, Yevgeny Prigozhin akiwa eneo lisilojulikana na kuchapishwa Agosti 21, 2023. Picha na REUTERS

Maafisa wa Russia wanasema kwamba, Yevgeny Prigozhin, kiongozi wa kundi la mamluki wa Rashia, alikua miongoni mwa abiria kwenye ndege ya kibinafsi ilioanguka Jumatano jioni kaskazini mwa Moscow.

Lakini hadi tunapotayarisha ripoti hakuna chombo cha nchi ya kigeni kilichoweza kuthibitisha kwa njia huru ikiwa kiongozi huyo alikua ndani ya ndege hiyo.

Msemaji wa mshauri wa Masuali ya Usalama wa Kitaifa wa Marekani, Adrienne Watson anasema, “sisi tumesikia ripoti hizo. Zikithibitishwa, basi haijabidi mtu yeyote kushanga.”

Shirika rasmi la habari la Russia linasema miili ya watu wanane imepatikana kwenye eneo la ajali.

Mapema mamlaka ya usafiri wa ndege Russia ilisema kwamba kulikua na majina ya watu 10 kwenye orodha ya abiria wa ndege hiyo iliyokua inatoka Moscow kuelekea St. Petersburg.

Ripoti zisizothibitishwa za vyombo vya habari zinasema ndege hiyo ilimilikiwa na Prigozhin, ambaye ni mwanzilishi wa kampuni ya kibinafsi ya kijeshi ya Wagner.

Kiongozi wa kundi la mamluki la Wagner, Yevgeny Prigozhin (kushoto) akiwa na wapiganaji wake huko Bakhmut, Mei 25, 2023.
Kiongozi wa kundi la mamluki la Wagner, Yevgeny Prigozhin (kushoto) akiwa na wapiganaji wake huko Bakhmut, Mei 25, 2023.

Mamlaka ya usafiri wa anga ya Russia, Rosaviatsia, imesema Prigozhin alikuwa kwenye orodha ya abiria. Hata hivyo, haikufahamika mara moja iwapo aliwahi kupanda ndege hiyo.

Shirika la habari la serikali ya Russia, Tass limewataja maafisa wa dharura wakisema kuwa ndege hiyo ilibeba marubani watatu na abiria saba. Maafisa wanasema wanachunguza ajali hiyo, iliyotokea katika mji wa Tver zaidi ya kilomita 100 kaskazini mwa Moscow.

Prigozhin, ambaye kundi lake binafsi la wanajeshi la Wagner lilipigana pamoja na jeshi la kawaida la Russia huko Ukraine, lilifanya uasi wa muda mfupi dhidi ya uongozi wa kijeshi wa Russia mwishoni mwa mwezi Juni. Na Ikulu ya Kremlin ikaeleza kwamba Prigozhin anapelekwa kuishi uhamishoni Belarus, na wapiganaji wake wangestaafu, watamfuata aliko , au wajiunge na jeshi la Urusi.

Video kwenye mtandao wa kijami Telegram zilizotangazwa na Wagner zilionesha picha -- ambazo AFP haikuweza kuthibitisha kwa njia huru -- za mabaki ya ndege ikiungua kwenye uwanja.

Siku ya Jumatatu, kulikuwepo na video iliyosambaa ikimuonyesha kiongozi huyo wa Wagner akiwa Afrika, ambako alisema ataongeza ushawishi wa kundi lake na kulifanya bara la Afrika kuwa "huru zaidi".

Forum

XS
SM
MD
LG